Karua Amshutumu Rais kwa Kukiuka Katiba Wakati wa Maandamano

AGOSTI 22, NAIROBI, KENYA. Kiongozi wa NARC Kenya Martha Karua amemshutumu Rais William Ruto kwa Kukiuka katiba kwa kuruhusu Wakenya wasio na hatia kudhulumiwa wakati wa maandamano dhidi ya serikali na kutoheshimu amri za mahakama. Akihutubia wanahabari hii leo jijini Nairobi, Karua alisema kwamba bado hakujakuwa na mabadiliko katika mfumo wa utawala chini ya utawala wa Ruto licha ya uteuzi wa hivi majuzi wa viongozi wapya. Katika hotuba yake, Karua aliapa kuendelea kuwahamasisha Wakenya dhidi ya utawala wa Rais Ruto hadi masuala yote yaliyoibuliwa na waandamanaji wanaoipinga serikali yatatuliwe.


PICHA: Kiongozi wa NARC-Kenya Martha Karua akishiriki kwa komgamano ya hapo awali

"Kwa kukosekana kwa jibu lolote la utawala wa Ruto, sisi kama Wakenya tutaungana na kushinikiza uwajibikaji. Tunaona kipindi cha kuongezeka kwa hali ya kutokujali," Martha Karua alifichua.
Karua pia aliahidi kuripoti Mkuu wa Nchi kwa mashirika ya haki za binadamu ya bara na kimataifa ikiwa ni pamoja na Tume ya Umoja wa Afrika ya Haki za Kibinadamu na Tume ya Umoja wa Mataifa (UN) ya Haki za Kibinadamu.

Karua alisisitiza kuwa kila tone la damu inayomwagika katika kupigania haki lazima ihesabiwe. Alitangaza mipango ya kuwasilisha malalamiko rasmi kwa AU na Tume za Haki za Kibinadamu za Umoja wa Mataifa, pamoja na vyombo vingine vinavyohusika. Karua alionya kuwa wataangazia ukiukaji huu kimataifa, haswa ikizingatiwa serikali kurejea mielekeo ya ukandamizaji. Pia alikosoa mtindo mpya wa ufadhili wa chuo kikuu, na kuutaja kuwa usaliti kwa wanafunzi wa Kenya. Kulingana na Karua, mabadiliko ya ufadhili yanazuia wanafunzi kupata elimu na kukiuka haki yao ya fursa za kujifunza.

Comments

Popular posts from this blog

Kenya Diaspora Alliance and KDA Welfare Association Host Impactful 4th Annual Social & Business Networking Event

Inaugural International Religious Freedom Summit Africa Launches in Nairobi

New Generation Aspirants Unveil Youth-Led Roadmap for a New Kenya